Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mmoja wa wanafunzi katika kituo cha Jimolojia Tanzania,Grace Charles akiendelea na ukataji wa madini huku akitumia kifaa maalumu.
Magret Joseph akiwa anaangalia kwa makini namna alivyokuwa akikata jiwe kwa kutumia mashine maalum.(picha zote na Woinde Shizza,Arusha)
Na Woinde Shizza,Arusha
Sekta ya madini nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu na wataalamu wa kufundisha namna ya ukataji wa vito vya madini hali inayosababisha kuuzwa kwa madini ghafi nje ya nchi na kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini na pesa nyingi kwenda nje ya nchi .
Hayo yameelezwa na mratibu wa kituo cha Jimolojia Tanzania,Musa Shanyangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika kituo hicho kinachotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito,ambapo wameanza kutoa mafunzo ngazi ya cheti kwa wahitimu 15 wakike ambapo chuo kipo katika halmashauri ya manispaa ya jiji la arusha.
Alieleza kuwa hivi sasa madini ghafi yanauzwa sana nje ya nchi kwa bei ya chini lakini kama wangeweza kuuza madini hayo yakiwa yameongezwa thaman na kuuzwa kwa bei ghali na kuwezesha fedha za kigeni kubaki nchini na kuongeza pato la taifa .
Shanyangi aliongeza kuwa hivi sasa wameanza kuwafundisha kozi ya miezi 6 kwa wanafunzi 15 wakike ambapo wanafadhiliwa na Arusha Women Foundation Fund iliyoko mjini ikiwa na lengo la kuwasaidia mabinti ili kuweza kusaidia sekta ya madini na kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalamu wa ukataji madini nchini.
Hata hivyo kituo hicho kinatarajia kuongeza wanafunzi mpaka kufikia 60 ili kuweza kuongeza ufanisi na kuweza kuboresha sekta hiyo ya madini ili kuweza kuongeza wataalamu ,pia wanamkakati wa kuweza kusomesha walimu wazawa ili kuweza kukidhi nakuwa na walimu na kupunguza gharama za kuchukua mwalimu kutoka nje yanchi ambapo hivi sasa wamemuajiri raia kutoka Sri lanka hali ambayo wanatumia gharama kubwa kumlipa mtaalamu huyo toka nje ya nchi.
Shanyangi aliwataka wadau mbalimbali nchini pamoja na wawekezaji wawekeze katika kufundisha wataalamu wazawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakataji na wataalamu nchini.
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi billion 1.2 na mashine mbalimbali za kituoni hapo zimegharimu zaidi ya milioni 450 za ukataji na kusafisha madini hayo.
Kwa upande wake mwanafunzi katika chuo hicho Bi.Joice Patrick alisema kuwa kupitia mafunzo hayo ya ukataji wa madini na ung'arishaji itawasaidia katika swala zima la ajira huku akiwataka wanawake kuchangamkia fursa hiyo "Ni fursa sasa kwa wanawake kujitokeza katika kazi hii na waione kama kazi zingine na si kuwaachia wanaume tu "alisema Joice.