Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira James Lembeli akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Kamati yake kwa Kipindi cha Mwaka 2014, Bungeni mjini Dodoma.
Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
KAMATI ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imesema kuwa hatua za Serikali za kupambana na ujangili nchini zimeonesha mafanikio makubwa.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe James Lembeli (pichani) alisema kuwa pamoja na mafanikio mengine hatua hiyo imefanikiwa kukamata silaha 2000.
Alisema hadi kufikia mwaka 2013, hali ya ujangili wa tembo ilikadiriwa kufikia tembo 30 kwa siku, lakini Serikali ilichukua hatua ya kuzuia na kutokomeza uhalifu huo kwa kuanzisha Operesheni Tokomeza.
“Pamoja na madhara yalijitokeza operesheni hiyo ilisaidia kuanza kupungua kwa kesi za ujangili wa tembo nchini” alisema Lembeli.
Hata hivyo aliishauri Serikali kuendelea na harakati za kupambana kwa nguvu zote na ujangili na kuweka wazi hali ya ujangili nchini ili wananchi na wadau wa hifadhi nchini waungane na Serikali.
Alifafanua kuwa baada ya Operesheni hiyo Serikali iliendelea kuchukua hatua zaidi kwa lengo la kutokomeza kabisa tatizo hilo. “Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuajiri askari wa wanyamapori zaidi ya 500 na wengine 300 waliajiriwa ikiwa ni askari wa kujitolea”alisema.
Hata hivyo aliishauri Serikali kuendelea na harakati za kupambana kwa nguvu zote na ujangili na kuweka wazi hali ya ujangili nchini ili wananchi na wadau wa hifadhi nchini waungane na Serikali.
Naye Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kampuni ya simu inayotoza gharama za maunganisho zaidi ya zile zinazodhibitiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Naibu Waziri Makamba alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde lililotaka kujua kwa nini kampuni moja inawatangazia wananchi kutoza gharama walizotumia.
Alisema TCRA inasimama ipasavyo kudhibiti huduma za mawasiliano kulingana na sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kudhibiti hujuma mbalimbali zinazofanywa na kampuni za simu.
Alifafanua kuwa katika kuimarisha udhibiti pamoja na hujuma hiyo, Kitengo Maalum kimeanzishwa ndani ya TCRA kinachoshughulika na malalamiko ya wateja yanayohusu huduma za mawasiliano.