Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BONDIA FRANCIS CHEKA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mwanamasumbwi maarufu Francis Cheka akiwa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kuhukumu ya miaka 3 jela.
Bondia Francis Cheka akipanda gari la polisi baada ya kuhukumiwa miaka mitatu kwenda jela.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Bondia Francis Cheka akiwa ndani ya gari la polisi 

Na Mwandishi wetu, 
Morogoro 
Bondia mashuhuri wa kulipwa nchini, Francis Cheka, ambaye maarufu kwa jina la SMG  amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Shilingi milioni moja kwa kosa la kumpiga meneja wa baa yake, Bahati Kibanda. 
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi  ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall. 
Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Mhe. Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo. 
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja. 
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini. 
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inasemekana ina mpango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>