Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiwa kwenye kizimba cha mahakama tayari kusomewa shitaka linalomkabili.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, akiwa kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, jana mchana wakati alipofika kusomewa shitaka la kesi yake ya jinai kwa kuwashawishi wafuasi wake kufanya fujo baada ya kutiwa mbaroni jana alipokuwa akiongoza maandamano ya wanachama wa CUF.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof Ibrahim Haruna Lipumba akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana alipofikishwa kujibu shitaka la kuhamasisha wanachama wa chama chake kufanya jinai.
Wanachama na Wafuasi wa CUF wakiimba nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiwatuliza wanachama na wafuasi wa chama hicho kuacha kelele katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana na kutoka nje ya Mahakama hiyo.
Gari za Polisi zikifanya doria maeneo mbalimbali ya jiji na maeneo ya Mahakama ya Kisutu ili kukabiliana na vurugu ambazo zingejitokeza.Picha na Sufiani Mafoto na Mroki Mroki