Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Gabriel Ng'osha akimkabidhi Bi. Masumbuko ambaye ni msimamizi wa wodi ya Sewa Haji namba 23 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pesa taslimu masaada wa laki moja na elfu kumi na nane (118,000) leo kwenye hospitali hiyo.
Emmanuel Nelson akiwa amelala kwenye wodi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Emmanuel Nelson mwenye umri wa miaka kati ya (30 - 35), ambaye ni mzaliwa wa Mbamba Bay, Ruvuma na ambaye wazazi wake wanaishi Dodoma, aliyekuwa anaomba msaada wa kutibiwa taya ambalo limevunjika. Leo amepatiwa masaada wa laki moja na elfu kumi na nane (118,000) kwa ajili ya matibabu kutoka kwa wasamalia wema kupitia blog yetu ikishirikiana na global publisher.