Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WATU WAWILI WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WATIWA MBARONI KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI ENEO LA DARAJANI ZANZIBAR MCHANA WA LEO

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Askari Polisi pamoja na raia waliokuwepo eneo la tukio wakiwa wamemzunguka mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi baada ya kumtia mbaroni leo mchana  katika eneo la darajani Jua Kali, Zanzibar.
 Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa chini ya ulinzi ndani ya Gari la polisi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mtuhumiwa mwingine ndani ya Gari.
Hii ndio gari waliyokuwa wakiitumia Watuhumiwa hao.

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi wametiwa mbaroni katika tukio la Ujambazi lililotokea leo mchana eneo la Darajani Jua Kali, Zanzibar  baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye hasira wakati walipokuwa wakiwakimbia Polisi.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walikua watatu na walitaka kuiba katika maduka na mawakala wa huduma za pesa yaliyopo eneo la Mnazi, baada ya kushtukiwa walikimbia na kufukuzana na Polisi hadi katika maeneo ya Darajani ndipo wananchi kwa kushirikiana na polisi wakawadhibiti na kuwakamata, hata hivyo mmoja alifanikiwa kutoroka na hadi sasa anasakwa na jeshi la polisi.


 Pia wapo baadhi ya wananchi wamelazwa hospitali ya Mnazi mmoja baada ya kupatwa na mshtuko kutokana na risasi zilizokuwa zikipigwa hewani na mmoja aligongwa na gari la watuhumiwa hao wakati wa kukimbizana na askari, Mmoja kati ya waliokamatwa na aliepata kipigo kikali anadaiwa kuwa ni jambazi sugu ambae alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kipindi kirefu,           ila kwa kuwa za mwinzi ni Arobaini,leo ndio katiwa nguvuni..


Watuhumiwa hao walikuwa na gari aina ya Toyota Noah lenye namba za Usajili T 736 CGT na walikamatwa baada ya gari lao hilo kushindwa kuendelea na safari baada ya kuingia kwenye njia ambayo hairuhusiwi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>