Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mtandao maarufu zaidi wa ujumbe wa simu, WhatsApp sasa unakuwezesha kuwasiliana na marafiki waliopo kwenye simu yako kwa kutumia laptop laptop na PC kwa mara ya kwanza.
WhatsApp imeboresha zaidi huduma yake ili wewe uendeleze mazungumzo yako uliyoanzisha kwenye simu unapokuwa unatumia laptop au computer yako.
Unapojiunga na huduma hii utakuwa ukipokea na kutuma ujumbe wa WhatsApp kwenye computer bila hata kushika simu hii ikiwa ina maana kuwa kinachoingia kwenye simu ndicho utakachokuwa ukikiona kwenye computer.
Bahati mbaya kama wewe unatumia iPhone hautaweza kufurahia huduma hii kwa kile wanachosema ni ‘Apple platform limitations. Lakini mambo ni mswano tu kwa wale wanaotumia simu za Android, BlackBerry, Windows au Nokia S60.
Ili ifanye kazi unachotakiwa kufanya ni kuupgrade kupata latest version ya WhatsApp kisha ingia kwenye web.whatsapp.com ukitumia browser ya Google Chrome itakayokuonesha QR code. Hakikisha pia simu yako imeunganishwa kwenye computer kwa njia ya USB.