Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wananchi wa manispaa ya songea mkoani ruvuma wamelalamikia tatizo la umeme lililoukumba mji wa songea kwa zaidi ya miezi mitatu sasa baada ya kuharibika mitambo ya kuzalisha umeme tangu Oktoba mwaka jana na kusababisha mgao mkali wa umeme katika mji huo.
Wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na ITV kuhusiana na tatizo la umeme katika mji wa songea na kusema tatizo hilo limesababisha maisha yawe magumu.
Meneja wa uzalishaji wa umeme wa nishati ya mafuta na gesi nchini
Mhandisi Gregory Chegelle amesema mafundi wanajitahidi kufufua mitambo iliyokufa na kwamba mji wa songea utarejea katika hali yake ya kawaida ya umeme mwezi februari mwaka huu watakapokamilisha matengenezo ya mitambo Hiyo.
CHANZO: ITV TANZANIA