Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Na Chalila Kibuda
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP, Agustine Lyatonga Mrema amesema hangoki ng’o katika nafasi ya uenyekiti TLP.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magomeni jijini Dar es salaam leo,Mrema amesema hajavunja katiba ya TLP hivyo yeye ni mwenyekiti halali.
Mrema amesema watu wanampiga majungu wakiwemo na UKAWA katika kuhakikisha TLP inasambaratika ,lakini hawataweza pamoja na kikundi hicho cha panya road.
Amesema kikundi kinachomtuhumu huwa kinaanza karibu na uchaguzi kikiwa kina nia ya kuiua TLP na wamepanga asishiriki katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo amesema wametangaza vyama vya upinzani vinavyounda UKAWA kuifuta TLP ambapo mamlaka hayo ya kufuta chama,UKAWA wanayatoa wapi.
Mrema amesema kupeleka uchaguzi mkuu mbele ilitokana na makubaliano kutokana na chama kuwa hakina fedha na msajili wa vyama vya siasa aliridhia kufanya hivyo na kufanya katiba hiyo kutoivunja.
CHANZO: MICHUZI BLOG