Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

DAZ BABA ADAI YUPO FRESH, ASEMA YEYE NA UNGA NI VITU VIWILI TOFAUTI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii wa muziki Daz Baba amekanusha madai kuwa afya yake ni mbaya kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na pombe.

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Daz amesema kuwa kuna watu waliamua kumpiga picha na kui-edit ili kumchafulia shunguli zake za muziki.
“Mimi mwenyewe nimeona kama uzushi flani hivi, yani ni uzushi, kwa sababu mimi nikwambie kitu picha waliopiga ni washikaji wa pale pale Morogoro na walifanya vile kutokana na mtu aliyewatuma ili kuharibu maisha yangu ya muziki, kwahiyo ndo hivyo kafanikiwa kuweka hiyo picha na ku-edit edit na kuweka mi kichaa sijui au naumwa sana, au naitaji msaada, lakini naomba mashabiki wangu waelewe kwamba Daz Baba bado yupo fresh na hizo stori nimezoea kuzisikia za uzushi uzushi tu, mimi nimesha waambia wasihukumu lakini wanaendelea kuhukumu hayo yote mimi namwachia mwenyezi mungu ambae amenipa nguvu,” alisema Daz

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Pia Daz amesema yeye ni rasta kwahiyo hawezi kutumia madawa ya kulevya huku akidai stori za kuwa anatumia unga zilianza muda sana.
“Dah! Yani hizo stori zilianza miaka sana, mimi ni rastafari, rastafari na unga ni vitu viwili tofauti kabisa, mimi naishi misingi ya kifamilia ya Tanzania, kama kundi langu Tanzaniano lilivyo na watanzania wenzangu walivyo, mimi issue za kujikweza siwezi , mimi naishi maisha ya watu wa kawaida na kujichanganya na watu wote, lakini mimi sivuti unga ni rastafari na ninaisha kirastafari,” alimalizia Daz.

CHANZO: BONGO 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>