Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipokewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe na Mbunge wa jimbo la Makambako Mh Deo Sanga(Jah People).
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipata maelezo kuhusu chanzo cha maji cha Fukurwa kutoka kwa mhandisi maji Inj. Steven Mkalimoto.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akipokewa na viongozi wa kijiji cha Lugenge.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla ( kulia ) akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Kifume. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba na kushoto ni Mbunge jimbo Makambako Deo Sanga.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amefanya ziara katika halmashauri ya Makambako na Halmashauri ya mji wa Njombe, ambako ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kijiji cha Kifume na Mtanga ambapo zaidi ya watu 6500 watapata maji safi na salama.
Aidha Mh Makalla ametembelelea chanzo cha maji cha Fukurwa kinachotumiwa na wakazi wa mji wa Makambako, ambako ameitaka halmashauri hiyo ikitunze vyema chanzo hicho cha maji.
Naibu Waziri huyo wa maji pia ametembelea mradi wa maji Lugenge ambao umemesimama kutokana na mkandarasi kutosamehewa kodi ya VAT.
Katika ziara hiyo, Mh Makalla amewaeleza wananchi kuwa, msamaha wa kodi umeshatolewa na fedha shilingi milioni 206 zimeshatumwa na mradi utaanza kutekelezwa mara moja.