Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015 kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akifungua duka rasmi.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akizungumza na vyombo vya habari kwenye ufunguzi wa duka hilo la vipodozi
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
Mmoja wa wateja waliofika katika duka hilo akitizama bidhaa
Muonekano wa duka la Zurii kwa ndani
Baadhi ya Bloggers wenzake waliofika kumpa support mwenzao kwenye ufunguzi wa duka la vipodozi
Baadhi ya Bloggers wenzake waliofika kumpa support mwenzao kwenye ufunguzi wa duka la vipodozi
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige leo amezindua rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.
Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hii”.