Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Milipuko hiyo baada ya kukamatwa mchana huu ikiwa ndani ya boksi
Kuna shehena kubwa ya milipuko ya hatari inayotumika kutengenezea Mabomu ya Kuvulia samaki na kutengenezea milipuko ya kupasulia miamba migumu imekamatwa eneo la Korogwe mchana huu wakati wa Jeshi la Polisi walipokamata Basi la KLM EXP lenye usajili wa namba T491 ARB kwa ajili ya Ukaguzi. Milipuko hiyo ambayo imesafirishwa kwa njia ambayo sio sahihi kutokana na hatari yake ya kuwa kulikuwa na abiria na kama Basi Lingetingishika zaidi Ingeweza Kulipuka .
Askari wa Jeshi la Polisi Katika Kituo cha Korogwe akikagua Milipuko hiyo
Basi hili limetumika kusafirisha Milipuko hiyo
Taarifa zaidi itakuijia hivi punde endelea kutufuatilia
Chanzo: Tanga Yetu Blog