Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Bushembe, wilayani Muleba, mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kumpiga mwanaye na kumpasua kichwa.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Dickson Wilson alimtaja mtu huyo kuwa ni Godfrey Joseph, mkazi wa Kijiji cha Bushembe na kwamba tukio hilo lilitokea Januari 3, mwaka huu.
Wilson alisema kabla ya kujinyonga, alimpiga mtoto wake wa miaka minane na kumjeruhi vibaya kichwani na kuhisi kuwa amemuua. Alisema hilo ni tukio la pili kwa marehemu kulifanya la kujeruhi watu wa familia yake, kwani awali alimpiga mkewe na kumchoma na spoku ya baiskeli iliyokuwa na moto sehemu zake za siri, kitendo kilichomfanya mwanamke huyo aondoke nyumbani.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rubya alikolazwa mtoto huyo kwa matibabu, Modesti Rwakahebula alisema wanaendelea kumtibu na hali yake bado haijatengamaa.
CHANZO: MWANANCHI