Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

BREAKING NEWS: MTOTO WA RAILA ODINGA AKUTWA AMEFARIKI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Fidel Odinga enzi ya uhai wake
Fidel Odinga ambaye ni mtoto wa mwanasiasa maarufu nchini Kenya Raila Odinga amekutwa akiwa amefariki nyumbani kwake eneo la Karen Jijini Nairobi . Chanzo hasa cha kifo chake bado hakijajulikana.
Fidel Odinga alizaliwa mwaka 1973 na pia ni mtoto wa kwanza katika familia ya Raila na Ida Odinga. Fidel ameacha mjane pamoja na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili. Baadhi ya wabunge wameanza kufika nyumbani kwa marehemu kutoa salamu za pole kwa ndugu wa marehemu.
Akiongea na waandishi wa habari  aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanae.
Maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mfanyibiashara huyo ambaye pia amekuwa akionekana katika ulingo wa kisiasa. Maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonyesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa jumamosi na alirudi mapema jumapili.

CHANZO: CITIZEN TV

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>