Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wanajeshi wa Indonesia wakiwa wamebeba majeneza yaliyobeba miili ya marehemu waliofariki kutokana na ajali ya ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea juzi
Jitihada za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia. Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo inapatikana.
Baadhi ya miili ya marehemu waliofariki kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 ikiwa kwenye meli tayari kwa kusafirishwa
Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya AirAsia.
Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofariki kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa wamepoteza fahamu baada ya kupewa habari mbaya zinazowahusu ndugu zao
Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini.