Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mashabiki wa kike wa Mombasa wakimsonga Diamond kwenye show yake mjini humo weekend iliyopita
Kunyanyashwa kwa wasanii wa Kenya, kumemfanya Diamond na waandaji wa show yake ya Mombasa weekend iliyopita kutupiwa lawama na wapenzi wa muziki nchini humo.
Mtandao wa Standard Media wa Kenya, umeandika kuwa kwenye show hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao, Diamond alitaka wasanii wengine wote waliokuwa watumbuize kwenye show hiyo na waliokuwa wamepangiwa kukaa naye kwenye VIP lounge, wakiwemo Susumila na Nyota Ndogo waondelewe.
Mashabiki wa Diamond mjini Mombasa wakifurajia show yake
Ilidaiwa pia kuwa Susumila na Nyota Ndogo walinyimwa maji ya kunywa na kwamba waliambiwa wanywe maji ya bomba kwakuwa maji ya kwenye chupa yalikuwa kwaajili ya Diamond peke yake.
Tukio hilo liliwafanya wasanii wa Mombasa waungane kuwalaani waandaji wa show hiyo ambapo VJ Delph alikataa kucheza muziki.
“Kama hili likiendelea, wapenzi wa muziki wa Mombasa watagomea show za Diamond mbeleni. Ni fedheha kwa wasanii wetu kutendewa hivyo nyumbani,” alisema Hassan Faisal wa Coastal Films.
Bongo5 haijaweza kuthibitisha mara moja taarifa hiyo kutoka kwa wahusika.