Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wakazi wa kitongoji cha Njedengwa kata ya makulu manispaa ya Dodoma wakingalia majina kwenye orodha ya wapiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa yaliyobandikwa ukutani jana.
Wakazi wa kitongoji cha Njedengwa manispaa ya Dodoma wakiwa kwenye mstari wakisubili kuingia kupiga kura za kucha viongozi ngazi ya serikali za mitaa, ambapo hata hivyo uchaguzi huo uliingia dosari katika kituo hicho baada ya kuzuka fujo na uchaguzi huo kusitishwa.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mpiga kura katika kitongoji hicho akiingiza karatasi ya kupigia kura kwenye boksi wakati kabla ya fujo kuzuka na uchaguzi huo kusitishwa mpaka j2 ijayo katika kitongoji cha Njedengwa Dodoma mjini.
Kamanda wa polisi wilaya ya Dodoma Mjini T. Malingumu akiwatangazia wananchi kuondoka katika kituo cha kupigia kura katika kitongoji cha Njedengwa West mara baada ya Afsa uchaguzi wa Manispaa ya Dodoma kutangaza kusitisha zoezi hilo baada ya fujo kuzuka katika kituo hicho ambapo sasa uchaguzi huo utafanyika siku 7 zijazo.
Polisi wakiimarisha usalama