Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UPDATES: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.

Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.

CHANZO: GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>