Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof Mark Mwandosya akisisitiza jambo kwenye mkutano wa mkuu wa 47 wa chama cha madaktari unaofanyika kwa siku 2 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Mhe, Kebwe Stevin Kebwe akizungumza jambo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha madaktari unaoendelea mjini Dodoma.
Madaktari ambao ni wajumbe wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) wakifuatilia jambo katika ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma walipokuwa kwenye mkutano wao wa 47.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof Mark Mwandosya na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Kebwe Stevin Kebwe wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa chama cha madaktari waliokuwa kwenye mkutano wao mkuu.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiwa nje ya ukumbi wa Pius Msekwa kwa ajili ya mapumziko kabla ya kuendelea na mkutano.