Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Keki ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), 'WEKEZA UVUNE'
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal. Picha zote na Cathbert Angelp Kajuna wa Kajunason Blog.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akishirikiana na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikabidhiwa zawadi kwa mchango wake anaoutoa katika jamii.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akiongea machache.
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikagua miradi mbali mbali inayoendeshwa na akina mama wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akionyeshwa jiko la kisasa linalopunguza matumizi. Pembeni kwake ni Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal katikati wakiongozwa na mwenyeji wao Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi leo Disemba 10, 2014 amezindua Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) itakayowawezesha watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwaajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Akiongea wakati wa uzinduzi Dk. Mengi aliwataka wanachama watumie fursa hii kupata mikopo kwaajili ya kutanua biashara zao, lakini pia wahakikishe wamejipanga mathubuti na kujiwekea malengo endelevu ambayo yataleta tija katika maendeleo yao.
"Nanawatia moyo wote, na pia ninapenda kuwapongeza sana na nawatakia kila lakheri" Alisema Mengi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba. Mpaka sasa tuna wanachama zaidi ya 200 hapa Dar es Salaam na tumejipanga kutanua wigo na kufungua matawi zaidi Kanda ya Kaskazini, mikoa ya Dodoma, Mtwara, Lindi, Mwanza hadi ifikapo mwezi wa tatu mwakani.
Lakini pia ipo miradi tuliyonayo yenye lengo la kuinua na kukuza chama hiki cha saccoss na kunufaisha wanachama wake.
Ofisi zetu ziko Oysterbay, Dar es Salaam hivyo nawakaribisha wanachama wapya kujiunga
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email annamatinde@gmail.com au 0754692994.