Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Vurugu za wananchi kufunga barabara katika eneo la Dumila zimesababisha madahara baada ya nyumba tano za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji katika mji mdogo wa Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuharibiwa vibaya na kuiba thamani za ndani.
Wakizungumza kwa masikitiko wamiliki wa nyumba hizo ambapo ni wafugaji wamelalalmikia kuwa hii ni mara ya pili wananchi kufunga barabara kisha kuvamia nyumba zao na kuziharibu na kusababisha hasara ambapo wameomba serikali kutenda haki kwani walihimizwa wapunguze mifugo na wawekeze katika majumba lakini kwa sasa wanachoshwa na uonevu unaoendelea na kuomba hatua zichukuliwe.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katika hatua nyingine mji wa Dumila umeonekana shwari hakuna vurugu zozote huku wananchi wakiendelea na shughuli zao ambapo baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo mama ntilie wamelalamikia vurugu zilizotokea zimesababisha hasara na kushindwa kuuza vyakula na maduka yalilazimika kufungwa kutwa nzima.
Kamanda Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hali nishwari katika mji wa Dumila na ulinzi umeimarishwa huku wakiendelea na uchuguzi wa waliohusika na tukio hilo na kuomba mamlaka husika kushughulikia na kumaliza mgogoro huo wa wakulima na wafugaji ili kuepusha madhara yanayotokea kwa wananchi.
CHANZO: ITV TANZANIA