Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mshindi wa pili wa BBAHotshots, Tayo Folarin
Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania Idris kwenye BBAHotshots, kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania.
Bilionea Ayiri Emami
Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo Ayiri Emami amempatia Tayo Folarin pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na BBAHotshots kwa mshindi wa kwanza. Tunawafahamu mabilionea wachache kutoka Nigeria wakiongozwa na Aliko Dangote, Emami leo ameonesha uwezo wake kwa kumpatia Tayo dola laki tatu na nusu (350,000/=).
Kiasi hicho ni backup kwa Tayo ambaye alionekana mnyonge sana usiku ambao Idris alitangazwa mshindi, hii itampa Amani ya kuendelea maisha na mpenzi wake na mtoto wake mmoja ambaye alizaliwa wakati Tayo akiwa ndani ya Jumba la Big Brother.