Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Anaye daiwa kuwa Daktari feki ,akiwa chini ya ulinzi Dar es Salaam jana, baada ya kuingia katika Taasisi ya Mifupa (MOI) akiwa amvalia nguo ya kazi na akiwa na kitambulisho cha kazi na kujifanya yeye ni Daktari wa Taasisi hiyo .Baada ya kukamatwa na askari alikutwa na vitu mbalimbali kama vile nyaraka za Serekali,(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Daktari feki aitwaye Dismas Macha amekamatwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa amefiwa.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema; “Tumekuwa tuna tatizo kubwa la kuletewa watu wanaokuja wao na kujitia ni madaktari wakiomba watu pesa, wakiomba waweze kupewa takrima na hata michango mingine na wamefikia hatua sasa ya kuwatapeli hata madaktari wenyewe kwa kuomba michango na vitu vingine“
Leo tumewaita Waandishi wa Habari kuwaeleza kisa cha mtu ambee amekuja na kujitia yeye ni Daktari wa sehemu ya taasisi na anaomba michango mbalimbali, na mtu huyu sii mara ya kwanza amekuwa akishikwa Muhimbili sehemu tofauti kwa wakati tofauti kwa hiyo tumewaita ili muweze kumtambulisha kwa jamii asiweze kudanganya watu wengine kwamba yeye ni Daktari”– Dk. Kiloloma.
Mwananchi mmoja ambaye alikuwa mmoja ya watu walishuhudia mtu huyo kukamatwa amesema; “Suala la Madaktari feki tatizo kubwa lililopo sio Madaktari feki kama hivyo kuna Mahakimu feki, Madaktari feki, ukishaona mahali popote anatokea mtu feki ujue kuna maslahi na tatizo kubwa linalojitokeza kwenye Hospitali ni ukifika Madaktari wenyewe halisi wanataka fedha ili wakuhudumie, kwa hiyo yoyote anaweza kujifanya feki kwa maana anakusanya fedha za Watanzania alafu anatoweka kwa hiyo anakuwa amekula fedha…“