Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu mwenezi wa Chadema, Kata ya Rigicha wilayani hapa, Bahati Mayala (37) amelazwa katika Hospitali Teule ya Nyerere baada ya kujeruhiwa kwa mshale wakati akitoka kwenye kampeni.
Tukio hilo lililotokea Desemba 5, aa 1:30 jioni katika Kijiji cha Kitembele limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali hiyo. Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Calvin Mwasha alikiri kupokewa kwa majeruhi akiwa na mshale mgongoni saa 6:00 usiku juzi na kufanyiwa upasuaji kutoa silaha hiyo ya jadi.
Mwasha alisema mshale huo ulikuwa umeingia inchi sita katika eneo la mapafu. Akizungumza na gazeti hili hospitalini hapo, Mayala alisema alipigwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Nikiwa njiani katika Kitongoji cha Ngayani ghafla nikasikia kitu kinakita mgongoni...nikaona watu wawili wanakimbia ambao niliwafahamu kwa nguo walizokuwa wamevaa na majina, wote wa Kijiji cha Kitembele. Niliposhika mgongoni nikakuta mshale, nikapiga kelele kuomba msaada,” alisema.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Alisema wananchi walikusanyika na kumpeleka kituo cha afya cha Natta, lakini walishindwa na kumpa rufaa kwenda hospitali hiyo. Kuhusu chanzo cha tukio, alisema ni kutokana na masuala ya kisiasa kwa kuwa siku hiyo kwenye mkutano wao kulitokea vurugu zilizosababishwa na wafuasi wa vyama vingine na wakati anarudi nyumbani akashambuliwa.
Kamanda wa polisi wa Wilaya ya Serengeti, Pius Mboko alikanusha madai ya kuhusisha siasa, akisema Mayala alijeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa wezi wa ng’ombe. “Si suala la siasa bali alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatilia wezi wa mifugo, ndipo akapigwa mshale wakati akiwa na watu wengine,” alisema.
“Watuhumiwa hawajakamatwa na tunaendelea kufuatilia,” alisema bila kubainisha ni ng’ombe wangapi walikuwa wameibwa na walikuwa ni mali ya nani. Alisema ng’ombe hao waliibwa katika Kijiji cha Monuna.