Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Ankal akimpongeza Binti yake Zahra wakati wa hafla ya Maulid ya Kumpongeza baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii imefanyika jana Nyumbani kwa Kaka wa Ankal,Tabata Kimanga jijini Dar es salaam.
Baba Mkubwa wa Zahra,Ismail Michuzi akiongoza dua ya kuwakumbuka ndugu waliotangulia mbele ya haki kabla ya shereha ya Maulid ya kumpongeza Binti Zahra alielamba Nondozz yake ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma,hivi karibuni.Kulia ni Ankal.
Zahra akijumuika na Mashangazi zake katika Maulid hiyo kwa picha zaidi bofya sma zaidi
Vijana wa Madrasa wakitoa burudani kwa Qaswida mwanana kabisa.
Ankal akisikiliza Jambo kutoka kwa Kaka yake,Macheka.
Dufu zikipigwa.
Ankal akiwatunza vijana wa Madrasa.
Vijana wa Madrasa wakiimba Qaswida kwa ustadi mkubwa.
Zahra na Mama zake wadogo.
Msimamo wa Qiyam.
Shangwe zatawala.
Binti wa Ankal,Zahra Muhidin Michuzi akiwa kaketi kwenye kiti chake tayari kwa kupongeza kwa kulamba Nondozz yake hiyo.
Ankal na Dada yake,Bi. Ndonya
Zahra katika picha ya pamoja na shangazi zake,Mama Zenna na Mama Fatma.
Michuzi Famili
Zahra na Marafiki zake.
Ankal akiwa na Wanae,Ramadhan (pili kushoto),Zahra (kulia),Karim (kushoto) na Sellah (alie na Ankal) wakati wa hafla ya kumpoza Zahra alielamba Nondozz yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii ilifanyika Tabata kwa Kaka wa Ankal ambaye ni Baba Mkubwa wa kina Zahra.
Zahra akiwa na Wadogo zake Kulwa na Dotto ambao ni watoto wa Kaka Mkubwa wa Ankal. Picha kwa hisani ya Michuzi Media Group