Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Una wazo zuri au kubwa la biashara, lakini huo ni mwanzo tu. Kuna habari za mtaani nyingi sana ukiona hivyo inawezekana ukafikiri kuwa utakuwa mtu uliyefanikiwa muda si mrefu sana. Hebu fikiria kwenye mpango wako na ujaribu kuangalia soko na maisha yako binafsi. Utahitajika kujua je mteja wako ni nani na uweze kuweka hiyo biashara ni kitu cha muhimu kwenye maisha yako. Bila ya kufanya hivyo uwezekano wa kufanikiwa ni mdogo;
Hebu jiulize maswali yafuatayo na ujue kweli wewe kama ni mjasiriamali
1. Je unatumia muda wako mwingi kwenye biashara yako?
Kama unatumia muda mchache kwenye biashara yako na inakuwa tu kama kamradi ka pembeni inaweza ikakusumbua kwani muda wako unahitajika sana. Unatakiwa uweke muda na malengo yako kwa ujumla kwenye biashara hiyo, inakuwa ngumu kutegemea biashara yako huku ukitumia muda mwingi kwenye kazi uliyoajiriwa. Unahitaji kujitoa kwa moyo wako wote kwenye biashara yako, inakuhitaji sana ili ikue.
2. Je kuna uhitaji wa bidhaa au huduma?
Unachotakiwa kuangalia je huduma yako au bidhaa yako ina wahitaji? Je ni kweli kwamba bidhaa au huduma yako inahitajika? Hata kama kitu unachouza ni cha tofauti au kinafanana na vingine lazima uonyeshe utofauti ili uweze kupambana kwenye soko la ushindani.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBODYA HAPA CHINI
3. Je uko tayari kukabiliana na shida?
Unapoanza biashara utakutana na shida na adha nyingi sana hata kama mpango wako wa biashara ni mzuri kiasi gani. Ni kitu kimoja kuwa na mpango mzuri na ni kitu kingine kujua shughuli za kila siku za hiyo biashara. Unatakiwa kujiandaa kwa mambo ambayo huyategemei na uwe na uwezo wa kujikwamua kutokana na hayo.
4. Je unajua kwa uhalisia mapato yako yatatokana na nini?
Unahitaji mfumo wa biashara, na uweze kujua wateja wako na unawezaje kutengeneza pesa baada ya kuwafikia. Kuwa na wazo zuni hakutaifanya biashara yako kufanikiwa. Unatakiwa kujua nani anahitaji bidhaa au huduma yako na uweze kuitathimini jinsi gani itakuwa hela halisi.
5. Je kufanya biashara ni kitu cha msingi na muhimu kwenye maisha yako?
Mashaka na wasiwasi wa familia unaweza kuharibu biashara yako, je uko tayari kutumia siku zote za wiki kufanya kazi bila kujali Jumamosi na Jumapili? Hakuna namna unaweza kujenga biashara yako bila kutoa sadaka katika sehemu fulani ya maisha yako. Kama hauko tayari kufanya hivyo inamaanisha utakutana na vitu vigumu sana na biashara yako haitafanikiwa.