Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WATU WAWILI WAMEFARIKI BAADA YA LORI LA MIZIGO KUPARAMIA PIKI PIKI BARA BARA KUU SIGIDA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. 


Watu wawili wamefariki papo hapo  baada ya lori la mizigo aina ya fuso,kuiparamia pikipiki ya magurudumu matatu maarufu kwa jina la  bajaji katika barabara kuu itokayo singida mjini kuelekea mwanza.
Akielezea tukio hilo kamanda wa polisi mkoani singida  ACP Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo limetoka siku ya tarehe mbili saa moja  na dakika hamsini usiku ,baada ya dereva wa gari la mistubishi fuso yenye usajili wa namba T.641 AVH ambaye alikuwa amelewa kuanza kuparamia magari mawili  kwa nyakati tofauti na baadaye kuigonga bajaji ambayo ilikuwa na abiria moja na dereva  na kusababisha vifo  vya watu wawili papo hapo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo  kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa singida Daktari Daniel Tarimo ,amesema wamepokea miili ya watu wawili moja ametambulika kwa jina la Thadei Antony  Maleo ambaye alikuwa dereva wa bajaji na mwili wa mwanamke ambaye haja fahamika kwa jina  anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya ishirini na tano na thelasini.
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali hiyo pamoja na kueleza kuwa dereva wa fuso alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi bila ya kuwa na tahadhari ,wameshauri madereva kuacha kutumia vileo pindi wanapokuwa katika kazi zao za kuendesha magari, kwani wamekuwa wakisababisha vifoo na hasara kwa uzembe. 
Katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka pamoja na kusherehekea sikuku ambazo zina kuja,kila mwaka kumekuwa na matukio ya ajali mbalimbali kutokana na uzembe wa madereva ,jambo ambalo lina changia  kupoteza maisha ya watu wasio kuwa na hatia na kuwasababishia ulemavu.

CHANZO: ITV TANZANIA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>