Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TEMEKE YANYAKUA UBINGWA WA KIKAPU TAIFA KWA KUIGALAGAZA MBEYA MJINI DODOMA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Mchezaji wa Temeke Baraka Said akiwapita mabeki wa timu ya Mkoa wa Mbeya na kufunga goli katika mchezo wa fainali uliofanyika jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
 Mchezaji wa timu ya kikapu ya mkoa wa iringa Jonsoni Chaga akipokea cheti cha kuwa mchezaji bora  wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa kikapu (Taifa Cup) kutoka kwa katibu wa chama cha kikapu taifa Saleh Zonga yaliyomalizika jana mjini Dodoma kwa Timu ya Temeke kuchukua ubingwa mashandano hayo.

 Nahodha wa Timu ya kikapu ya wanawake mkoa wa Dodoma Imelda Hango  akipokea Kombe la ubingwa wa mashindano hayo toka kwa katibu wa cha kikapu Tanzania (TBF) Salehe Zonga
Nahodha wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Temeke wanaume Frank Semkoko akipokea kombe la ubingwa wa mashindano ya taifa kwa mchezo wa kikapu (Taifa Cup) Toka kwa katibu wa chama cha mchezo huo Saleh Zonga.


NA JOHN, DODOMA

TIMU ya Mkoa wa Kimichezo wa Temeke  imetawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Mashindano ya Taifa kwa mchezo wa Kikapu Taifa Cup mara baada ya kuipa kichapo Mbeya kwa vikapu 85-43 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Temeke ambayo iliingia fainali baada ya kuichapa Iringa kwa vikapu 88-50 katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza juzi,huku Mbeya ikiifunga Arusha kwa vikapu 69-61 katika nusu fainali ya pili zote zikifanyika katika uwanja wa Jamhuri.

Katika fainali hiyo iliyokuwa ya upande mmoja kwa Mbeya kuzidiwa kila idara na Temeke ambayo ilikuwa ikiongozwa na kikundi cha kidedea kilichokuwa kikiishangilia timu hiyo mwanzo wa mechi hadi mwiasho hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa vikapu 43-14.

Temeke ambayo ilikuwa ikiongozwa na mchezaji hatari Baraka Saidi ambaye alifunga vikapu 35 pamoja na nahodha wao na mchezaji wa timu ya Taifa Frank Simkoko waliwabana vilivyo Mbeya ambao walikuwa wakiongozwa na Hamfrey Mwakatundu na Joginda Msai ambaye alikuwa akihaha uwanja mzima hadi filimbi
ya mwisho ya mwamuzi Temeke waliibuka na ushindi wa vikapu 85-43.

Katika fainali ya Wanawake timu ya Dodoma iliichapa Mbeya kwa vikapu 41-27 katika pambano lilokuwa na ushindani huku mchezaji kutoka Dodoma Imelda Hango akifunga vikapu 30 kati ya 41 walivyofunga timu yake huku Mbeya wakiongozwa na Zaitun Hamis wakiweza kuichachafya vilivyo ngome ya Dodoma.

Mchezaji bora wa Mashindano kwa upande wa Wanaume alikuwa ni Jonson  Chaga kutoka Iringa huku kwa upande wa Wanawake alikuwa ni Imelda hango kutoka Dodoma na huku Mfungaji bora aliibuka Jonson Chaga kutoka Iringa huku kwa wanawake akiwa ni Imelda Hango.

Akifunga Mashindano hayo Katibu wa Chama cha Kikapu Nchini (TBF)Salehe Zonga alisema amefurahishwa na viwango vilivyooneshwa na Wachezaji kutoka katika mikoa ya Kigoma na Kagera huku akiahidi kuvitunza vipaji
vilivyoonekana katika mashindano hayo.

‘’Pamoja na kuwa na timu chache lakini tumeweza kuyafanya mashindano ya mwaka huu yakawa na mvuto kutokana na kuwa na vipaji kutoka katika mikoa ya pembezoni kama Kagera na Kigoma nani alijua kama huku kuna vipaji,’’alihoji Zonga.

Mashindano hayo yalianza Desemba 24 na timu zilikuwa katika makundi mawili ambapo kundi A lilikuwa na timu za Mbeya,Kigoma,Ruvuma, Morogoro huku kundi B ni timu za Temeke,Arusha,Kagera na wenyeji Dodoma,Bingwa katika Mashindano hayo akijinyakulia Kikombe.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>