Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WAWILI WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI AKIWEMO MMILIKI WA MATEI LOUNGE MKOANI DODOMA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na. SYLVESTER ONESMO wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mnamo tarehe 30/12/2014 majira ya 18:30hrs huko njia panda ya NARCO barabara kuu ya Morogoro – Dodoma Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma gari lenye namba za usajili T. 213 DAR Toyota  Mark X, likiendeshwa na HASSAN s/o HUSSEIN, mwenye umri wa miaka 42, mzigua, Mkazi wa Dodoma likiwa na abiria wanne wakitokea Morogoro wakielekea Dodoma liligonga kwa nyuma gari lenye namba za usajili T. 963 BRC Leyland Daf lililokuwa na tela lenye namba T. 708 ASP likiendeshwa na TUMAINI s/o JOSIA, mwenye umri wa miaka miaka 23, mjaluo, Mkazi wa Mbagala rangi tatu Mkoani Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu wawili pamoja na majeruhi watatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MATEI s/o JOHN MMASI, mwenye umri wa miaka 32, Mchaga, Mfanya Biashara wa Matei Lounge iliyopo Mkoani hapa ambaye alifariki njiani alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na JOSHUA s/o OGUDA, mwenye miaka 32, wakili wa kujitegemea, Mkazi wa Kikuyu kusini aliyefariki akiwaanaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa Dodoma.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Kamanda MISIME amewataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni BOSSI s/o NGASA @ SEBASTIAN Mwenye umri wa miaka 28, mzigua mkazi wa Makole Mmiliki wa Blog ya Bossngassa ambaye amelazwa wodi namba 1, JUMA s/o ZUBERI mwenye miaka 23, mkazi wa Nzuguni ambaye amelazwa wodi namba 11 pamoja na HASSAN s/o HUSSEIN, mwenye miaka 35, mzigua, Mkazi wa Dodoma aliyekuwa dereva wa gari dogo ambaye amelazwa wodi namba 1 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Kamanada MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua taadhari kulikochangiwa na mwendokasi. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>