Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini Leo ukitokea Nchini Malaysia.
Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Wa http://www.josephatlukaza.com
Msiba wa Marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa leo uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam umepelekwa Kwake Sinza na Hatimaye Kesho Kutakuwa na Misa ya kumuombea marehemu na hatimaye Mwili wa Marehemu kupumzishwa Katika Nyumba yake ya Milele Katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe