Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PICHA: YALIYOJIRI JANA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiliongoza Bunge mjini Dodoma leo,wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mtu mmoja kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kupatikana akisambaza Ripoti ya (ESCROW) ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Sheria Baada ya Hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia.
Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia akiwa amekaa na Hasimu wake wa Siasa jimbo la Vunjo Mhe.Agustino Mrema wakimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda.


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO MATUKIO ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana ya wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda. Aliye valia gauni la njano ni Mbunge wa Busanda Mhe.Lolesia Bukwimba.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda.
Mbunge wa Busanda Mhe. Lolesia Bukwimba (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya juu ya ugeni wake wa wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sofia Simba (kushoto) akifurahia jambo na Mhe.Anna Mkinda wakati wakitoka katika kikao cha Bunge. Picha zote na Deusdedit Moshi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>