Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari leo siku ya Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni.
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa5.00 asubuhi.
Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam.