Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwili wa mshiriki wa Miss World aliyepotea siku chache kabla ya kusafiri kwa ndege kwenda London kwaajili ya mashindano hayo umepatikana.
Miss Honduras, Maria Jose Alvarado, 19, na dada yake Sofia Trinidad, 23, wamepatikana jana wakiwa wameuawa. Maria – aliyeshinda taji la Miss Honduras – alipotea akiwa na dada yake baada ya kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yao Alhamis iliyopita.
Honduras, nchini maskini yenye watu milioni nane pekee ni miongoni mwa nchi zenye uhalifu zaidi duniani.