Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Soko la vinyago lililoko karibu na ofisi ya CCM wilaya ya arusha limeteketea kwa moto na kusababisha Hasara ya Mabilioni ya Fedha.
Wananchi na wafanyabiashara ambao vibanda na mali zao zote zimeteketea wamesema walianza kupata taarifa za moto huo usiku na walivyofika walikuta kila kitu kimeteketea.
Wananchi hao wamesema inakuwa vigumu kubaini chanzo cha moto huo kwani katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na chama cha mapinduzi(CCM)hakuna umeme wala chanzo chochote cha moto.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aidha wananchi wameiomba serikali na vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi na kuchukua hatua ya kuwasaidia kwani ni janga kubwa kwao hasa ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa wanaendesha Biashara zao kwa kutegemea mikopo.
Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia leo.
Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo