Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAHAKAMA YA ILALA YAFUTA AMRI YAKE YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WANAODAIWA KUKIFUNGA KITUO CHA TIBA ZA ASILI NA MBADALA CHA FOREPLAN HERBAL CLINIC CHA BUNGONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


 Wakili Lucas Kamanija (kulia), anayemtetea Dk. Juma Mwaka katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanadaiwa kukifunga kwa makufuli  Kituo cha Tiba za Asili cha ForePlan Herbal Clinic kilichopo Ilala Bungoni, kinachomilikiwa na Dk.Mwaka, akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana, mara baada ya kusikiliza kesi hiyo ambapo Mahakama hiyo imefuta amri iliyotolewa awali ya kuwakamatwa  watuhumiwa tisa kutoka katika wizara hiyo. Kesi hiyo imeharishwa hadi Novemba 20
 Wanasheria wa Serikali wakibadilishana mawazo nje ya mahakama hiyo wakati wa kusikiliza kesi hiyo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Wakili Lucas Kamanija (katikati), akizungumza na wanahabari
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo

Dotto Mwaibale

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imeifuta amri yake ya awali ya kuwataka wafanyakazi tisa wa Wizara ya Afya kufungua makufuli waliyoyafunga kwenye kituo cha  tiba za asili na mbadala cha Foreplan Herbal Clinic eneo la Ilala Bungoni.

Uamuzi huo umeleotolewa  na Hakimu Mkazi John Msafiri wa mahakama hiyo, Adolf Sachore. Kabla ya uamuzi huo kutolewa, Wakili  Charles Kamanija anayemtetea Dk. Juma Mwaka aliiomba mahakama hiyo isiusome kwa sababu hakimu aliyeuandaa Msafiri hakuwepo.

Hakimu Sachore aliyatupilia mbali maombi hayo na kuusoma uamuzi huo ambapo aliifuta amri ya awali iliyotolewa na mahakama hiyo ya kutaka wafanyakazi hao tisa kufungua makufuli kwenye kituo hicho na wasimuingilie katika biashara yake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Amri hiyo ya awali ilitolewa, baada ya Wakili  wa Serikali, Karim Rashid kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuiomba mahakama hiyo kuiondoa na kuruhusu wao kuunganishwa  na kuwa sehemu ya wadaiwa kwenye kesi hiyo.

Baada ya kutolewa kwa maombi hayo, Hakimu Sachore alikubaliana na maombi ya Karim na kuyatupilia mbali maombi ya Dk. Mwaka kwa maelezo kuwa hayana msingi.

Katika maombi ya Dk. Mwaka kupitia wakili wake, Charles waliwasilisha pia ombi la kuzuia maofisa hao kuingilia shughuli za mteja wake hadi kesi ya msingi waliyofungua mahakamani hapo itakapomalizika.

Kwa mujibu wa kesi hiyo ya madai namba 204 ya mwaka 2014, imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa maombi ya zuio Novemba 20, 2014.

Dk. Mwaka vile vile anaiomba  mahakama iwaamuru washtakiwa wakafute maandishi waliyoyaandika kwenye kuta za kliniki hiyo yanasosomeka; ‘Kituo hiki kimefungwa na Wizara ya Afya leo 06/11/1914’ pamoja na kutomwingilia katika biashara yake mlalamikaji.

Kutokana na uamuzi huo, wakili wa mlalamikaji Charles Kamanija alidai nje ya eneo la  mahakamani kuwa viongozi wa  serikali wameshindwa kutii amri ya mahakama ya kuja mahakamani na kwamba wanapanga utaratibu wa kupinga umuzi huo. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>