Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kwa muda mrefu watumiaji wa Instagram wamekuwa wakishindwa kurekebisha (kuedit) caption wanazoweka kwenye picha wanazopost kwenye Instagram. Matokeo yake ni kuwa baadhi ya picha hizo tumekuwa tukiziona zikiwa na maelezo yaliyokosewa na mtumiaji kushindwa kufanya chochote.
Instagram sasa imeongeza kifaa cha kuedit maelezo.
Updates mpya ya app hiyo kwenye iOS na Android inawapa watumiaji uwezo wa kuedit caption pamoja na kuongeza location baada ya kuwa wamepost picha. Kampuni hiyo imesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikipata maombi kutoka kwa watumiaji wengi kuhusu kuwepo kwa uwezo wa kuedit caption.
Button ya kuedit ipo upande wa chini wa picha na unaweza kuanza kufanya hivyo sasa kama utaupdate app yako.