Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

RATIBA YA KUAGA MWILI LEO NA MAZISHI YA ROBERT VICTOR LENGEJU

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro na Dar es Salaam inapenda kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu ROBERT VICTOR LENGEJU na Familia ya LENGEJU kuwa kijana wao mpenda aliyefikwa na umauti Novemba 10, 2014 katika Hospitali ya TMJ baada ya kuugua kwa muda mfupi anataraji kuzikwa kesho Alhamisi nyumbani kwao Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro.

Kipera ipo mbele kidogo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Mwili wa marehemu ROBERT LENGEJU, utaagwa leo kuanzaia saa 6:00 mchana baada ya Misa katika Kanisa Katoliki Msimbazi Dar es Salaam na baade jioni kusafirishwa hadi Morogoro.

Kesho Novemba 13 2014, kuanzia saa 5:00 Asubuhi taratibu za mazishi zitaanza nyumbani kwao KIPERA kwa misa takatifu na maziko.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>