Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na Wanaume Family, Said Fella amesema amejipanga kugombea ubunge wa jimbo Kigamboni, Dar es Salaam kwenye uchaguzi mkuu mwakani.
Fella ameuambia mtandao huu kuwa anachukua uamuzi huo ili kutetea watu wake katika eneo lake ambao anaona wanakosa huduma kutokana viongozi kutosimama vizuri. “Kama Mungu akinijalia uhai mrefu nina uhakika nitagombea katika jimbo la kigamboni,” amesema Fella.”Ndipo ninapoishi mimi. Naomba Mungu iwe 2015, sitaki kuchelewa.”
Fella amesema kujiingiza kwake kwenye siasa hakutaathiri shughuli zake za kusimamia wasanii na tayari amejiandaa kwa hilo.
“Mimi naendesha familia yangu nina maduka yangu na yanaenda vizuri, lakini bado nafanya muziki na unaenda vizuri. Kwa sababu maduka yangu nimefungua kabla hata muziki wa bongo fleva sijaujua na mpaka sasa hivi yapo. Wasanii wangu wa TMK wapo.
na Bongo 5