Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kuna makala moja nilikuwa naisoma inahusu kijana mmoja ambaye alimuuliza mkufunzi wake hivi: Nina shida, inaonekana watu hunisahau mara moja. Ingawa mimi ninakutana nao na ninakumbuka kuwa nilishakutana nao lakini wao hata hawakumbuki kama walishawahi kukutana nami. Nifanyeje?”
Kukumbukwa ni muhimu sana hasa kwa mfanyabiashara, kwani watu hawatanunua kwako kama hawakukumbuki au kama hawakujui kama upo. Mambo ya kufanya ili uweze kukumbukwa kibiashara zaidi;
1. Tafuta vitu vya kufanana
Siku zote tafuta kitu gani mnafanana na wateja wako au watu unaokutana nao. Watu watakwamini na kufanya na wewe biashara kama wanaona kuna kitu mnafanana au mnahusiana kwa namna moja ama nyingine. Kama labda wote mnatokea, kijiji kimoja , mmesoma shule moja au wote mnapenda kitu fulani. Hapo uwezekano wa kukumbukwa ni rahisi sana. Hata ukifanya vipi au ukatapeli vile vile ni rahisi pia kukumbukwa. Unapotafuta vitu vinavyofanana usifanye makosa ambayo yataathiri biashara yako.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
2. Tafuta kujua wateja au watu ha wanapendelea kufanya nini
Wengi wetu tunamaliza maongezi baada ya salamu tu. Lakini unaweza ukaendeleza maongezi kwa kujua wanafanya nini na ujue zaidi. Na wewe mwenyewe tafuta neno rahisi au sentensi rahisi ambayo itakufanya ukumbukwe pamoja na biashara yako. Mfano, kama unafanya biashara ya kutafuta maneno unaweza kusema “Biashara yangu ni kusaidia biashara zingine kufahamika zaidi” kauli hiyo inamfanya mtu kujiuliza mara nyingi au kutaka kujua zaidi kuhusu unachofanya.
3.Weka Sahihi yako ya Tofauti
Hapa haimaanishi kwenye makaratasi, bali je biashara yako ina utofauti gani na biashara nyingine katika ubora na muonekano wake? Vile vile hata uvaaji wako unavaaje unapokuwa mbele ya wateja wako? Muonekano wako na Bidhaa yako vinajenga taswira fulani ambayo inaweza kufanya ukumbukwe au usikumbukwe.
4.Jifunze kuuliza maswali mengi zaidi
Ingawa hii inaonekana kana kwamba watu watakushangaa, mara nyingi waongeaji sana hukumbukwa zaidi kuliko watu wakimya. Uliza maswali ya msingi na ambayo yatamfanya mtu aone unafikiria zaidi na kuwafanya kwamba unajali na kutaka kujua kuhusu shughuli zao.
5.Tafuta sababu ya kuwafuatilia
Kama watu hawakukumbuki ni kwamba wewe huwapi fursa ya wao kukukumbuka. Ni vigumu sana kumkumbuka mtu uliyekutana nae mara moja tu na kufanya maongezi kwa muda mfupi. Kitaalamu mtu husahau baada ya masaa 24 kitu chochote atakachoambiwa hivyo kama hakikirudia au kuandika sehemu inakuwa ngumu sana kukumbuka. Hivyo unaweza kuwafuatilia kwenye twitter, linked in na penginepo na hata kuwapigia simu mara moja moja kwa namna hiyo unaanza kujenga uhusiano nao taratibu.
Zaidi ya hayo kuna vitu vingi vya kufanya ili kuboresha muonekano wako pamoja na biashara unayofanya ili iwe na mvuto mkubwa na watu kukukumbuka zaidi.