Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PICHA: CHADEMA YAAPA KUINGO'A CCM MKOANI DODOMA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mkurugenzi wa Oganaizeshen na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wakazi wa mkoa wa Dodoma waliohudhuria Mkutano wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Barafu.
 Mkurugenzi wa Oganaizesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila akionyesha wananchi fomu ya kupigia kura(haipo pichani) ambayo inamtaka kila mpigaji kuchora nembo ya chama husika cha mgombea anayetaka kumpigia kuchagua iliyosainiwa na Waziri mkuu.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Dodoma wakigombania kununua kadi za CHADEMA mara baada ya mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Barafu jana.

Wakazi wa mkoa wa Dodoma wakiinua mikono kama ishara ya kukubaliana na kilichokuwa kikisemwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni na mafunzo wa CHADEMA Benson Kigaila aliyekuwa kwenye mkutano wa chama hicho uliondaliwa kimkoa na kufanyika katika uwanja wa Barafu.

Na John Banda,Dodoma

WAKAZI wa Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanakipigia kura  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika chaguzi zote ilikuweza kupata Maendeleo ambayo yamekuwa yakikwamishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)

 Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Oganaizesheni na ufundi Chadema Taifa na Msimamizi wa Kanda ya Kati ,Benson Kigaila katika mkutano wahadhara uliondaliwa na Chadema kwa kushirikiana na Vyama vya Upinzani ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi Nchini(UKAWA)katika viwanja
vya Barafu mkoani hapa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika mazingira ya uongozi wa sasa wa CCM ni bora kumwacha nyoka aina ya kifutu au kobra aende zake kuliko kuiacha CCM iendelee kutawala na Chama kitakachowaokoa wakazi wa Dodoma ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambacho kinasimamia haki na maslahi ya Taifa .

“Niwaombe wakazi wa Dodoma mchague Chama cha kweli ambacho ni chadema kitawaondolea matatizo yenu yote likiwemo tatizo la kuvunjiwa nyumba zenu na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu’’

‘’Serikali hii sio sikivu kwa wananchi wake tatizo la CDA linawasumbua wao wanaanzisha Mamlaka mpya ya inayosimamia ujenzi  Kigamboni na Kibaha pwani wakati ni zaidi ya miaka 40 Dodoma bado haijawa makao makuu sasa Chagueni Chadema muondokane na dhana hii ya kuthulumiwa haki zenu ambazo ni za msingi’’

“Niwaambie kitu CCM wamekuwa ni wanyonyaji wa mji wa Dodoma pamoja na kupigiwa kura nyingi na wakazi wa hapa jamani huu ni wakati wa sisi kulishika hili jahazi ili tuuboreshe mji huu nitapiga kambi ya siku 10 ili niing’oe CCM hapa kwenu na hili linawezekana kama mtakuwa pamoja nami’’

‘’Majiji yote yanamechukuliwa na Chadema angalia Arusha,Mwanza,Ubungo,Dodoma na yenyewe inataka kuwa jiji wakati ndio huu kabla haijawa jiji Chadema tuwe tumeishaishika ili tuwape huduma muhimu ambazo mnatakiwa mpewe,’’alisema Kigaila

Benson akizungumzia kuhusu taratibua za uchaguzi wa serikali za Mitaa uliosainiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema hilo ni changa la macho kwa watanzania lakini pia hata CCM itawagharimu kutokana na kuweka kanuni ambazo haziwezi kutekelezeka .

Mbali na hilo alisema kuwa kanuni zilizowekwa kuwa mpiga kura anatakiwa kuchora nembo ya chama anachokipigia kura huo ni uhuni hivyo ameahidi kuwa yupo tayari kumpa Pinda kiasi cha Sh.Bilioni moja kama anaweza kuchora nembo zote za vyama na halmashauri husika kwa muda wa nusu saa.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>