Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la Polisi kikosi cha wanamaji limekamata jahazi moja ambalo linatoka nchini Irani ambalo linadaiwa kuwa na shehena ya dawa za kulevya.
Akizungumza kuhusu tukio hilo kamanda wa kikosi hicho kamanda Mboje Kanga amesema walilikamata jahazi hilo baada ya kulitilia shaka na ndani yake wapo watu.
Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa za kuleya nchini Godfrey Nzowa amesema mapambano bado yanaendelea japo zipo changamoto nyingi na kuongeza kuwa robo tatu ya vigogo wa dawa za kulevya wamekwisha kamatwa.