Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

HAYA NI MAMBO 6 AMBAYO HUPASWI KUYASEMA KWENYE INTERVIEW YA KAZI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Mchangiaji wa mtandao wa Forbes, Ken Sundheim ambaye pia ni mtaalam wa masuala ya ajira anaeleza vitu sita ambavyo hutakiwi kuvisema kwenye interview ya kazi.


1. “Nataka kuwa na biashara yangu”– Pamoja na kuwa ni jambo jema kuwa na ndoto hiyo, mameneja waajiri hutafsiri tofauti kabisa. Hawaoni kama una nia ya kufanya kazi bali ni tishio kwao. Hii ni kwasababu waajiri wanahofia unaweza ukaiba taarifa za muhimu.
Kitu cha mwisho ambacho kampuni inataka ni kumfundisha mpinzani wake wa baadaye.


2. Vipi mnanionaje? Waajiri wanataka kuwaajiri wale wanaojiamini. Unapouliza mrejesho au feedback wakati wa usahili, unajiweka katika hatihati ya kuhisiwa vibaya. Unaonekana pia dhaifu kwa kuuliza swali hili.

3. ‘unajua’ eeeh’- maneno haya yanaonesha udhaifu katika kujikita na kinachoendelea. Pia maneno hayo wakati mwingine yanaonesha ukilaza na kutokuwa na interest.
These interjections can also hurt your tone of voice and ability to persuade as most interviewers will respond positively to vocal consistency. It can bore the audience when you attempt to elaborate on your answers. Finally, saying “um” and “like” will lead to the interviewer shying away from their main points and losing brevity in their statements,” anaelezea.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



4. “Kampuni yenu inafanya nini? Hakuna njia nzuri zaidi ya kumkera anayekufanyia interview zaidi ya kuuliza swali hili. Huonesha dharau ya waziwazi na kuwa hauna nidhamu ya kazi. Kufanya utafiti wa vitu muhimu kuhusu kampuni inaonesha kuwa uko vizuri katika kazi yako, unavutiwa na nafasi hiyo na umejianda kuipata kazi hiyo.

5. “Nataka kuingiza kiasi x cha shilingi.” Somo muhimu katika kushawishi ni kwamba huwezi kutegemea wengine kukupa kile unachotaka. Kama unataka kuwa na ushawishi zaidi, kuwa na tabia ya kushughulikia matakwa ya wengine kabla ya kuuliza kuhusu yako. Waombaji wa kazi wazuri huwapa mameneja waajiri kile wanachotaka kwanza, kisha huzungumza kuhusu fedha baadaye. Matokeo yake, huishia kupata fedha nyingi zaidi.

6. Interview hii itadumu kwa muda gani? Watu wote hupenda kujisikia ni wa muhimu na hata anayekufanyia usahili pia. Waoneshe kuwa sio kipaumbele na utakuwa umepoteza muda wako kwakuwa hili litawakata stimu!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>