Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Picha ya kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kimegundulika maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Leonard Thomas amegundua kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar.
Akizungumza na GPL Lenard alisema: "Nilikuwa naenda kuchoma moto taka ndipo nikaona kitu kama chuma kizito kama bomba ila kikanishangaza kiko kipekee nikiwa bado na shangaa mwenzagu akaja kuniambia kuwa ni bomu ndipo nikawajulisha polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kuweka ulinzi wakati wakisubiri wataalamu wa mabomu wafike. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar, Suleiman Kova amethibitisha kuwa kitu hicho ni bomu!
Gari la uchafu likiwa linaenda kuchukua uchafu eneo la tukio.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wananchi wakiwa eneo ambalo kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kimeonekana.
Askari polisi wakiwa eneo la tukio.
Leonard Thomas aliyekuwa anaenda kuwasha moto kwenye takataka zilizokuwa juu ya kitu hicho kinachosadikika kuwa ni bomu