Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.
Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea mahabusu ya Segerea.
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz amefikishwa mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.
Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka yake.
Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.
Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo itakapotajwa.