Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) BAADA YA KUSAINI WARAKA WA USHIRIKIANO KWENYE KIWANJA CHA JANGWANI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 -Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
 Waendesha bodaboda ambao ni wafuasi wa Ukawa wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya Jangwani.
 Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.
 Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa  kwenye mkutano huo.
Vijana wa chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com
 Hakika leo ni siku ya kihistoria siku ambayo itakumbukwa na vizazi vijavyo ni siku ya kusaini MoU kati ya vyama vinne vya kisiasa yaani CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI NA NLD.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles