Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kuna taarifa zilitoka jana jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
Imefahamika ni kweli msanii huyu amekamatwa jana mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano na kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kuusikiliza hapa.