Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kumbis akiwa hospitalini.
MZEE Mohamed Kumbis Said (60) mkazi wa Vingunguti Dar, amejikuta akiishi maisha ya kuombaomba baada ya kupata ajali na kuvunjika miguu yake yote kitendo kilichomfanya ashindwe kufanya kazi zake kama zamani na kushinda akiwa amelala.
Sehemu ya miguu iliyovunjika.
Mzee Kumbis alipata ajali hiyo Oktoba 4 mwaka jana maeneo ya Ilula-Iringa baada ya kukutana uso kwa uso na malori mawili na kisha kuyakwepa na kugonga karavati na yeye kuumia huku abiria zaidi ya 50 wakipona.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Sehemu ya miguu iliyovunjika.
“Niliokoa abiria wengi sana, nakujikuta nikiumia mimi mwenyewe na raia mmoja wa kigeni aliyevunjika kidole, nilizimia kwa saa 10 na nilipozinduka nilijikuta niko wodini na nimeshonwa nyuzi 8 kichwani, kiukweli niliumia sana, mguu wangu wa kulia umevunjika mara 4 na pia umekuwa mfupi, wa kushoto umevunjika mara moja.
Maisha ya mzee Kumbis kwa sasa ni magumu sana akiishi katika nyumba ya kupanga huku familia kubwa ikimtegemea, mbaya zaidi mkewe aliyekuwa anamsaidia naye alifariki baada ya yeye kuvunjika miguu ,’’ alisema Kumbis.
‘’Napenda kuwaomba watanzania kunisaidia kwani inahitajika milioni 15 ili nikafanyiwe oparesheni ya kurekebishwa miguu yangu ili kurudi katika hali yangu kama zamani ,nakufa huku najiona, hata niliofanya nao kazi hawana msaada na mimi , ni kama nimetelekezwa, kwa yoyote anayehitaji kunisaidia awasiliane nami kwa namba 0654 092796 au 0766 279670 jina Mohamed Kumbis Said.
NA GPL