Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WANASHERIA KUTOKA ULAYA NA MAREKANI WANAOIWAKILISHA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED WAMEIBUA UKWELI JUU YA MGOGORO UNAOIKUMBA KAMPUNI YA KUFUA UMEME HAPA NCHINI YA IPTL.

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Wakili kutoka Uholanzi Dk.Camilo Schutte akifafanua jibu lake kwa waandishi wa habari jijini Arusha jana.
Wakili kutoka Marekani Chris Provenzano naye akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa swali.
Mwanahabari Faustine Kapama akiongoza mahojiano hayo.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Wanasheria wa kampuni hiyo wakipitia baadhi ya taarifa kwenye mtandao wakati wakijibu maswali ya wanahabari. Kushoto ni Wakili wa Kitanzania wa Kampuni ya VIP, Resipius Didace.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya VIP,  James Rugemalira (kulia), akiwaelekeza jambo mawakili hao. 
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya VIP,  James Rugemalira (kulia) akiangalia moja ya taarifa zinazohusu Kampuni ya IPTL akiwa na  wakili wake kutoka Uholanzi. 
Wakili Camilo kutoka Uholanzi, akifafanua jambo mbele ya wanahabari. Kulia ni Wakili Didace.
Mawakili hao kutoka ulaya na Marekani wakiteta jambo wakati wakitoa majibu kwa wanahabari.
Mwanahabari Jamila Omary akichukua taarifa hiyo.
Mpiga picha Dotto wa Kituo cha Channel Ten akichukua kumbukumbu za mahojiano hayo. Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

Wanasheria kutoka Ulaya na Marekani wanaoiwakilisha Kampuni ya Uwekezaji ya VIP Engineering and Marketing Limited wameibua ukweli juu ya mgogoro unaoikumba Kampuni ya Kufua Umeme hapa nchini ya IPTL. 

Katika kueleza ukweli huo, Wanasheria hao waliongozwa na maswali yafuatayo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Arusha leo. 


 Miongoni mwa maswali waliyoulizwa Wanasheria hao yalikuwa yanahusu mada zifuatazo: 


 1. Kueleza historia fupi ya mgogoro wa IPTL tangu ulivyoanza hadi sasa. 


 2. Kueleza msimamo wa VIP Engineering and Marketing Ltd kuhusu Akaunti Maalumu (Escrow Account) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 


 3. Kueleza kwa nini Akaunti Maalumu (Escrow Account) ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. 


 4. Kama hisa za IPTL zingetolewa kwa mtu mwingine zaidi ya PAP, kwa mfano, Benki ya Standard Chartered; Je ni kweli kuwa mnunuzi yeyote wa hisa za IPTL angeweza kuwa na haki juu ya Escrow Account? 


 5. Baadhi ya wahisani wametangaza kusitisha kuunga mkono bajeti ya Serikali kwa kuwa wanaamini kwamba kuna ufisadi kwenye fedha zilizokuwa kwenye Escrow Account. Upi ni ushauri wao kwa serikali ya Tanzania juu ya suala hilo. 


 6. Je Benki ya Standard Chartered inayo madai yoyote dhidi ya IPTL na kwenye akaunti maalumu (Escrow Account). 


 7. Kama wanauamini mfumo wa mahakama za Tanzania 


 8. Nini msimamo wako kuhusu madai yanayotolewa eti kwamba Mahakama za Tanzania zinanuka rushwa. 


 9. Baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini zimetangaza kuwa Benki ya Standard Chartered imefanikiwa kupata amri ya mahakama huko Uholanzi kukamata mali za VIP Engineering and Marketing Ltd zilizoko katika nchi hiyo. Je kuna ukweli juu ya taarifa hizo.


 TUTAWALETEA MAJIBU YA MASWALI HAYO KWA KIREFU NA KWA UFASAHA BAADAYE.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>