Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MPIGADEBE ANUNUA MBUZI WAWILI NA KUWAPELEKA KITUO CHA WATOTO YATIMA KUTOA MISAADA MKOANI MBEYA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 

 Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi wilayani mbeya amenunua mbuzi wawili na bidhaa nyingine za aina mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na kuzipeleka kwenye vituo vya watoto yatima kama zawadi huku akiwaasa watoto hao kutoshawishika kwenda kupiga debe kwenye vituo vya mabasi.
 Mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi, Anganile Mwamuluma Andrea ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ameushangaza umma wa wakazi wa mbeya baada ya kuamua kununua mbuzi wawili, mchele, maharagwe, sabuni, mafuta ya kupikia na mahindi na kupeleka bidhaa hizo katika vituo viwili vya watoto yatima ambako amezitoa kama zawadi kwa watoto hao, huku akiwaasa kutoshawishika kujihusisha na kazi ya kupiga Debe kwenye vituo vya mabasi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Walimu wa watoto hao wameeleza kushtushwa na kitendo cha mpigadebe huyo, lakini wakasema kuwa ni mfano Bora wa kuigwa kwa vijana wanaofanikiwa kukumbuka mazingira walikotoka, huku wakiwahimiza wazazi kuongeza upendo kwa watoto wao ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini.
Baadhi ya watoto ambao wamepokea msaada huo, wamemshukuru mpigadebe huyo na kuwataka watu wengine kupata funzo la kuthamini na kuwapenda watoto ikiwa ni pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri ya kujitegemea.

CNANZO: ITV TANZANIA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>